Latest Events

TAARIFA KWA UMMA

IDARA YA UHAMIAJI HAIJATANGAZA NAFASI ZA KAZI KATIKA SIKU ZA HIVI KARIBUNI 

UFAFANUZI JUU YA “UZUSHI” ULIOENEA KWENYE TOVUTI NA MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU IDARA YA UHAMIAJI KUTANGAZA NAFASI ZA KAZI

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na uvumi unaoenezwa kupitia baadhi ya tovuti na mitandao ya kijamii kuhusu Idara ya Uhamiaji kutangaza nafasi za ajira kwa ngazi ya Konstebo na Koplo. Tunaamini uvumi huo unaenezwa na watu au kikundi cha watu kwa nia ya kujipatia maslahi yao binafsi au kwa malengo wanayoyafahamu wao.

Kufuatia kuwepo kwa taarifa hizo, Idara ya Uhamiaji inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

  1. Idara ya Uhamiaji haijatangaza nafasi zozote za ajira katika kipindi cha hivi karibuni, hivyo tunawaomba wananchi wasirubuniwe au kushawishiwa na mtu yoyote kutoa kitu chochote ili waweze kusaidiwa kupata kazi Idara ya Uhamiaji;

  1. Taarifa za kutangazwa nafasi za kazi zilizotolewa kupitia blogu husika na Mitandao ya kijamii si za kweli, bali ni uzushi uliofanywa na watu au kikundi cha watu kwa malengo wanayoyajua wao;

  1. Idara ya Uhamiaji, kama Taasisi ya Serikali hutangaza nafasi za ajira kwa uwazi kupitia Magazeti, Televisheni na Tovuti yake ambayo ni www.immigration.go.tz

  1. Idara inalaani na kukemea vikali watu au kikundi cha watu kinachotoa taarifa za upotoshaji kuhusu Idara kutangaza nafasi za kazi kama ambavyo imeripotiwa kwenye baadhi ya tovuti na mitandao ya kijamii.

Imetolewa na;

KITENGO CHA UHUSIANO,

MAKAO MAKUU, IDARA YA UHAMIAJI,

BARABARA YA LOLIONDO, KURASINI,

S.L.P 512, DAR ES SALAAM.

1 Jully, 2017.

www.immigration.go.tz

News and Events

PRESS RELEASE (NEW)

KUISHA KWA ZOEZI LA UHAKIKI JAMHU...

TAARIFA KWA UMMA

IDARA YA UHAMIAJI HAIJATANGAZA NAFASI ...

Facebook Fan Page

Visitors Counter

TodayToday110
This WeekThis Week3034
This MonthThis Month24866
All DaysAll Days103154
Visitors Online 18