TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA - 2023

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa Mamlaka niliyonayo chini ya Kanuni Namba 11(1) ya Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, natangaza nafasi za Ajira Mpya za Askari wa Uhamiaji kwa Vijana wa Kitanzania wenye sifa zifuatazo:-

1. SIFA ZA MWOMBAJI

 1. Awe ni raia wa Tanzania;

 2. Awe amehudhuria na kuhitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) au Jeshi la Kujenga

  Uchumi (JKU) waliopo Makambini au tayari amerudi Uraiani;

 3. Awe hana ajira au hajawahi kuajiriwa na Taasisi yoyote Serikalini;

 4. Awe na Cheti cha Kuzaliwa;

 5. Awe na Kitambulisho cha Taifa au Nambari ya Utambulisho iliyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA);

 6. Awe na siha njema ya mwili na akili iliyothibishwa na Daktari wa Serikali,

 7. Awe hajawahi kutumia Dawa za kulevya;

 8. Asiwe na Kumbukumbu au Taarifa zozote za kuhusika katika masuala au matukio ya uhalifu au jinai;

 9. Asiwe na alama yoyote au michoro (Tatoo) katika mwili wake;

 10. Awe hajaoa au kuolewa wala kuwa na mtoto;

 11. Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Nne awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 23, Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Sita na Stashahada awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 26 na Mwombaji mwenye Elimu ya Shahada awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 30.

 12. Awe tayari kufanya kazi za Idara ya Uhamiaji mahali popote Tanzania.

 13. Awe tayari kujigharimia katika hatua zote za ufuatiliaji na uendeshwaji wa zoezi la

  Ajira.