Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapenda kuwajulisha wageni na wadau wote kuwa haijasitisha utoaji wa Visa kwa wageni kwenye vituo vya kuingilia na kutoka nchini.
Hata hivyo, Idara ya Uhamiaji Tanzania inashauri wageni wote ambao wanapenda kutembelea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madhumuni mbalimbali kuomba Visa kabla ya kuingia nchini kupitia mfumo wa Visa mtandao (e-Visa)