Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia vijana waliochaguliwa kujiunga na Idara ya Uhamiaji; ambao walitakiwa kuripoti kwenye mafunzo katika Chuo cha Uhamiaji cha Raphael Kubaga kilichopo mkoani Tanga tarehe 03 Aprili, 2024 kuwa, wanatakiwa kuripoti rasmi chuoni hapo tarehe 15 Aprili, 2024 kuanzia saa 02.00 asubuhi hadi saa 08.30 mchana...