TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO - FEB, 2023
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia vijana wafuatao ambao wamechaguliwa kujiunga na Jeshi la Uhamiaji kuripoti Chuo cha Uhamiaji cha Raphael Kubaga kilichopo Boma Kichakamiba, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga siku ya Jumatano tarehe 01 Machi, 2023 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana. Kwa walioomba na kuchaguliwa kupitia Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, wanatakiwa kuripoti Afisi Kuu Zanzibar siku ya Jumatano tarehe 22 Februari, 2023. Atakayeripoti chuoni baada ya muda uliotajwa hatapokelewa...