Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia Vijana waliofaulu usaili na kuchaguliwa, kujiunga na Chuo cha Uhamiaji Raphael Kubaga kilichopo Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, kuwa wanatakiwa kuripoti tarehe 03 Aprili, 2024 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana. Yeyote atakayeripoti Chuoni baada ya muda huo hatapokelewa. Aidha, Kwa wale wote walioomba na kuchaguliwa kupitia Afisi ya Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar..